Icône d'Elisabeth de la Trinité - Carmel de HarissaEe Mungu wangu ! Utatu Takatifu ambaye naabudu ! Nisaidie nijisahau kabisa, ili nikae ndani yako, niwe kama mutu aliye kuwa katika umilele. Fanyiza hata kitu moja kisiniangaishe na kisiniondoe ndani mwako ; ila kila dakika nipeleke mbali kabisa ndani ya fumbo lako. Tuliza moyo wangu, uwe mbingu yako ; makao yako mapendelevu na mahali pa pumziko lako. Fanyiza nisikuache ndani mwangu peke yako bali nikae pamoja nanyi nafsi yangu yote. Niwe kama mtu mwenyi imani, mwenyi kuabudu na kujitolea kwa kazi yenu ya uumbaji.

Ee Kristu Mpenzi Wangu ! Ulisulubiwa kwakutipenda sisi ! Natamani kuwa mpenzi wako wa kiroho! Nataka kukusifu, na kukupenda hata kufa. Ila mimi ni mzaifu! Na ndiyo maana nakuomba univike na nafsi yako, ufananishe moyo wangu na moyo wako. Unizamishe katika uwepo wako, unijaze ili maisha yangu yakutambulishe kwa watu. Njooni ndani mwangu kama mwenyi kuabudiwa, kama mfinyanzi na mwokozi.

Ee Neno la milele ! Kinywa cha Mungu wangu ! Natamani kupitisha maisha yangu nikikusikiliza. Nataka kuwa mwanafunzi mwema ili nifundishwe yote nawe. Tena, kupitia usiku wote, utupu wote, uzaifu wote, nataka kukudokelea macho na kuketi chini ya mwanga wako mkuu. Ewe Nyota yangu Mpendelevu! Univute kabisa ili nisije ondoka kamwe katika mwanga wako.

Ewe Moto unayeteketeza ! Ewe Roho wa mapendo ! Njooni ndani mwangu kama umlisho wa Neno la Mungu, niwe kwake umutu wa zaidi ambamo atafanya upya Fumbo lake lote. Na We Baba Mwema ! Unielekeze uso wako mimi kiumbe chako kizaifu, unifunike na kivuli chako. Uone ndani mwangu mpenszi wako.

Ewe Utatu Mtakatifu ! Heri yangu, Upekee usio na mwisho na ambamo najipoteza ! Najitolea kwenu kama mnyama ambaye amenaswa. Kaeni ndani mwangu ili nami nijizike ndani yenu, nikingojea kwenda kutazama kwa makini katika mwanganza wenu lindi la ukubwa wenu.